Commons:ISA Tool/sw
Ongeza data ziliyopangwa kwa faili kwenye Commons kwa njia rahisi na ya kufurahisha!

ISA ni zana ya kufurahisha, ya lugha nyingi, ya kwanza ya uchangiajimdogo, ambayo hurahisisha (vikundi vya watu wasio na uzoefu) kuongeza data iliyopangwa kwenye picha kwenye Wikimedia Commons.
Ukiwa na ISA, unaweza kuchagua seti iliyofafanuliwa awali ya picha kwenye Commons kisha uwaombe wachangiaji 'kuziwekea kishikizo' hizi kwa taarifa zinazohusu data ziliyopangwa kwa lugha nyingi. Pointi huhesabiwa kwa kila mchango, na kwa hivyo inawezekana kuandaa mashindano ya 'kuweka vishikizo' au mashindano ya michango midogo au mashindano na ISA.
ISA iliundwa awali ili kutoa maelezo bora zaidi ya lugha nyingi na muundo wa Wiki Loves Africa. Lakini pia imeundwa ili kuwa muhimu kwa mashindano yote ya Mashindano ya Wiki Lovess X, na hatimaye ilikusudiwa kwa faili zote za media kwenye Wikimedia Commons.
ISA ilitengenezwa kama ushirikiano kati ya Wiki In Africa, Histropedia na mradi wa Data Zilizopangwa kwenye Commons. Ni majaribio ya GLAM kwa Data Zilizopangwa kwenye Wikimedia Commons. Uwezeshaji na mawasiliano unaoendelea kwa Zana ya ISA unafanywa na timu ya Wiki In Africa.
Namna inavyofanya kazi?
Zana hii imeundwa kuwa seva ya mashindano madogo!
Wanawikimedia (andaaji) wanaweza kuunda kampeni za kuboresha aina moja au maalum za picha kwenye Wikimedia Commons, ndani ya muda fulani. Taarifa hutolewa kwenye chombo cha kugeuza kampeni hii kwa urahisi kuwa shindano mdogo.
Kisha wanawikimedia (washiriki) tumia zana kuboresha maelezo ya pichayaliyojumuishwa katika kampeni iliyotajwa.
Zana hutoa takwimu zinazoruhusu kutambua wachangiaji bora wa kampeni husika kwa wakati halisi. Maelezo ya ushiriki hutolewa katika muundo mzuri wa kuona ambao unaweza kutumika moja kwa moja kujumuisha katika ripoti ya mratibu au kutumiwa kuwasilisha matokeo ya shindano kwenye mitandao ya kijamii, na kugeuza kampeni kuwa chombo cha mawasiliano!
Data kuhusu ushiriki pia inapatikana kwa kupakuliwa katika muundo wa cvs kwa matumizi yoyote zaidi ya takwimu.
Tembelea Menyu ya ISA kwa Wachezaji na Waratibu kwa ajili maelezo zaidi.
Usitawisho wa Zana
Toleo la kwanza la zana lilitangazwa wakati wa Wikimania 2019.
Zana hii iliboreshwa zaidi wakati wa mradi wa R&D mnamo 2022-23. Tazama Mradi wa R&D 2022-2023: Uwekaji wa vishikizo kwa msaada wa kompyuta
Hackathon iliandaliwa Januari 2024 ili kuboresha zana : Hackathon ya Wiki Mentor Africa 2024.
Msimbo wa chanzo cha zana unaweza kupatikana hapa:
- Phabricator ISA : https://phabricator.wikimedia.org/tag/isa/
- Vinjari msimbo: https://github.com/wikimedia/labs-tools-Isa
- Changia kwenye msimbo: https://gerrit.wikimedia.org/r/#/admin/projects/labs/tools/Isa
- Saidia kutafsiri zana: https://translatewiki.net/wiki/Translating:ISA
ISA kwenye Habari
Diff article (13 Machi 2024)
Hackathon ya Wiki Mentor Africa 2024 (19-21 Jan 2024)
GlamWiki thread on Twitter kuhusu Data Zilizopangwa kwenye miradi ya majaribio ya Commons (Machi 2020)
Kuitambulisha ISA - zana nzuri ya kuongeza data ziliyopangwa kwenye Commons (Nov 2019)
Jarida la GLAM (Aprili 2019)
Tutorial Videos
* A Tutorial video about how to use ISA Tool as a participants. (This video explains what structured data is, what ISA is, and how to add structured data using ISA.)
* A tutorial video about how to create ISA campaign as a campaign manager.
Viungo Vinavyohusiana
ZANA: https://isa.toolforge.org/
TAFSIRI: Ukurasa wa Mwanzo kwenye TranslateWiki
PHABRICATOR: Ukurasa wa mradi wa Phabricator
TOOLHUB: ISA kwenye ToolHub
TAKWIMU: Commons:ISA Tool/Stats
Baadhi ya mafanikio ya ISA..

- ISA ilipokea zana nzuri zaidi Tunzo ya WikidataCon 2019!

- ISA ilipokea Tuzo ya Zana Nzuri Zaidi' katika Wikimania 2024, kundi Eggbeater!
Jina "ISA" linamaanisha nini?
'Isa' ni neno la lugha ya chiShona la 'weka' au 'weka mahali', lakini pia linaweza kutumika kama kifupi cha Uongezaji Kasi Uliyoundwa na Taarifa, Nyongeza za Muundo wa Taarifa na mengineyo.
Sifa za Wasanidi Programu
- Wamehusika katika maendeleo ya awali

- Florence Devouard, development process lead, Wiki In Africa
- Islahaddow, communications lead, Wiki In Africa
- Eugene Egbe, Developer
- Navino Evans, Technical manager, Histropedia
- Sean McBirnie, Designer, Histropedia
- Mark Holmquist, Development advisor
- Sandra Fauconnier, mentor and SDC liaison, Wikimedia Foundation
- Wamehusika katika usitawisho wa ziada (2022-23)
- Beat Estermann - Project Coordinator
- Eugene Egbe (contractor WMSE) - Software Development
- Matthias Ruediger (BFH) - Software Development
- Navino Evans (contractor WMSE) - Software Project Manager / Software Architect
- Sebastian Sigloch (SWITCH) - Representative Funding Institution
- Sebastian Berlin (WMSE) - Software Development
- André Costa (WMSE) - Coordination on the side of WMSE
- Florence Devouard (contractor WMSE) - Community Outreach
- Wamehusika katika usitawisho wa ziada (2023-24)
Mifano ya Watumiaji wa Zana ya ISA

Mifano ya watumiaji ifuatazo ni ya kubuni ili kukusaidia kufikiria jinsi zana ya ISA inaweza kukusaidia kama mratibu wa kampeni au mchezaji, na kusema kweli, kuna mawazo mengi ya ubunifu zaidi ya haya.
Mfano
: Edit-a-thon ya Wiki Loves Africa 2014 nchini Nigeria.
Jumuiya ya Wanaijeria hupanga kampeni kwa kutumia ISA ili kuboresha maelezo ya picha kutoka Wiki Loves Africa 2014. Mratibu huanzisha kampeni ya warsha ya uhariri siku moja ya Jumamosi. Jamii moja pekee ndiyo itakayoorodheshwa kwenye zana : Category:Images from Wiki Loves Africa 2014 in Nigeria.Washiriki hushindana ili kuboresha maelezo ya picha katika saa maalum. Mratibu hufuatilia takwimu za ushiriki katika muda halisi. Washindi 5 bora wa washiriki wanatangazwa, na zawadi hutolewa. Chapisho la Facebook hushiriki matokeo, na washiriki wanaweza kupakua data za ushiriki kwa uchambuzi zaidi.
Mfano
: French-speaking Editors Drive
Wahariri wanaozungumza Kifaransa huanzisha kampeni ya kuboresha maelezo yaliyopangwa ya picha za Wiki Loves Africa 2015 kutoka nchi zinazozungumza Kifaransa.
Mfano
: Kampeni ya Uhamasishaji wa Mazingira
Shirika la kimataifa la mazingira linapanga kuendesha kampeni kwa kutumia ISA ili kuboresha taarifa kuhusu data kwa picha zinazohusiana na masuala ya mazingira. Kampeni hii inalenga kuhusisha washiriki duniani kote katika kuweka lebo na kuboresha maelezo ya picha za viumbe vilivyo hatarini kutoweka, uchafuzi wa mazingira na juhudi za uhifadhi. Waratibu huunda kampeni, huweka jamii mahususi, na kuhimiza washiriki kuchangia katika kuongeza ufahamu kuhusu changamoto za mazingira.
Mfano
: Mpango wa Tofauti za Lugha
Mpango wa utofauti wa lugha umezinduliwa ili kuboresha taarifa kuhusu data kwa picha zinazoangazia matukio ya kitamaduni, mila na maeneo muhimu ya kihistoria. Waratibu walianzisha kampeni zinazolenga jumuiya za lugha mahususi ili kuboresha data iliyoundwa kwa lugha nyingi kwenye Wikimedia Commons. Washiriki huchangia kwa kuongeza maelezo mafupi na na kinachoonyeshwa katika lugha mbalimbali, ili kuboresha uwakilishi wa ulimwengu wa maudhui ya kitamaduni.
Mfano
: Ushiriki wa Taasisi ya Elimu
Taasisi ya elimu inashirikiana na ISA kushirikisha wanafunzi katika kampeni ya uboreshaji wa taarifa zinazohusu data. Taasisi inaunda kampeni inayozingatia picha zinazofaa kwa mtaala wake, kuwahimiza wanafunzi kushiriki katika kuweka vishikizo na kuelezea maudhui ya elimu. Kampeni inakuza ushirikiano kati ya wanafunzi na waelimishaji, na kuunda uzoefu muhimu wa elimu huku wakichangia Wikimedia Commons.
Mfano
: Shindano la Kupiga Picha kwa Msimu
ISA hutumika kwa shindano la upigaji picha la msimu, ambapo washiriki huchangia katika kuboresha taarifa zinazohusu data kwa picha zilizopigwa katika misimu mahususi. Waratibu hupanga kampeni za misimu tofauti, wakiwahimiza washiriki kuongeza maelezo ya kina na vitu vinavyoonekanakana kwenye picha. Shindano hili huleta shauku miongoni mwa wapiga picha na wapenda taarifa zinazohusu data, na hivyo kuunda ushirikiano mzuri wa jamii.